“Ardhi ya nchi ndio mali yetu, wenzetu hawa wana matatizo ya ardhi, serikali itambue ardhi hii ni kwa ajili ya Watanzania, hivyo serikali ikafanye tafiti mipakani na kama kuna ardhi imeshanunuliwa kinyemela na wenzetu hawa irudishwe,”
- Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM)
Pengine kuna kila sababu ya kuhofu.
Japo naafiki maneno ya Mheshimiwa hapo juu ila naona panahitajika nyongeza kwamba serikali pia idhibiti ardhi kwa ufanisi zaidi siyo tu kutokana na hofu za kuporwa na watu wa nchi jirani.
Mara nyingine ni vigumu kuielewa mantiki iliyo nyuma ya kuwashupalia majirani kuhusiana na ardhi ilhali wananchi wa kawaida wanaendelea kuhamishwa kwa nguvu au kunyang’anywa ardhi na wageni wa kutoka mbali pamoja Watanzania wenyewe.
Kwa mujibu wa habari hii kuna ununuzi wa kinyemela wa ardhi uliofanywa Rufiji.
Kadhalika makampuni ya kimataifa yanayozalisha mazao ya nishati kwa madai kuwa tutapata faida kama vile fursa za ajira, fursa za masoko kwa bidhaa na mazao, upatikanaji wa nishati vijijini na mijini, kukua kwa uchumi wa wananchi, kupungua kwa umasikini, na kupungua kwa wimbi la nguvu kazi kukimbilia mijini.
Wakati tunawakalikia majirani, baadhi ya viongozi na Watanzania wengine wenye nafasi wamekuwa wakichukua ardhi kwa hila.
Basi likisikika suala la shirikisho la Afrika Mashariki,
Hivi bila ya mchakato wa shirikisho, masuala ambayo tunaweza kuyashikia usukani na ambayo tunapaswa kuyadhibiti
1 comments:
I am doing research on blogs and I would like to send u few questions. Can u help? If you are willing please send me your email, because it is not shown in your blog. My email is "njonjo.kweja@gmail.com" I am njonjo mfaume, tutorial assistant at School of Journalism of the University of Dar es Salaam, and MA Journalism student at Makerere University.
Post a Comment