FIFA imetoa ranking za timu. Nakubali Hispania kuwa juu, ikifuatiwa na timu kadhaa kama inavyoonyeshwa hapa.
Timu za Afrika Misri na Ghana zinatuwakilisha kwenye chati juu juu. Cha ajabu ati timu kamaAustralia iko juu zaidi ya Ghana ambayo ilikwenda mbali zaidi kwenye kombe la dunia, ilishiriki vizuri tu kwenye mashindano ya kombe la Africa nk.
kama kawaida nilipokuwa naitafuta Tanzania nilibofya moja kwa moja ukurasa wa mwisho na kuanza kurudi mwanzo. Sikutarajia kuikuta nchi yetu kwenye kurasa mbili za mwanzo.
0 comments:
Post a Comment