Wednesday, October 21, 2009

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI – Tanzania

Tanzania imepanda kwa chati kwenye takwimu mpya zilizotelewa muda mchache uliopita.. Ipo kwenye alama ya 62 kati ya nchi 175 zilizoangalia kwenye chati ya Reporters Without Borders For Press Freedom.

Chati hiyo inaangalia uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari katika nchi 175, na kiwango ambacho mamlaka za nchi zinathamini, zinahakikisha au kiwango ambacho zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na jitihada zinazofanywa na mamlaka katika nchi ili kuhakikisha kuwa uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari unaheshimiwa.