Friday, May 09, 2008

WAGONJWA JEURI

Tuko tayari kutumia jeshi letu la majini kukusanya waliopoteza maisha, waliopotea, na kuweka hali sawa. Lakini ili kuweza kufanya hivyo, utawala wa kijeshi lazima uturuhusu kuingia nchini humo.
2008

Tunaghafirishwa na serikali ya Myanmar kwa inavyojivutavuta kupokea na kukubali usaidizi wetu. Ni wazi uwezo wa serikali hiyo siyo mkubwa kuweza kukabili hali iliyopo, ambayo ni janga"
2005

"Madaktari wetu wanao uzoefu wa kimataifa na wanaijua lugha ya kiingereza ambayo itawawezesha kuwasiliana na waathirika. Tupo tayari, tunasubiri tu majibu ya serikali ya Marekani."

Friday, May 02, 2008

MANDELA BADO NI GAIDI MAREKANI

"Afrika ya kusini ni nchi ambayo tuna mahusiano mazuri nayo kwa sasa, ni jambo lanalotia aibu kwamba inanibidi kuondoa kikwazo cha pingamizi la kibali cha kuingia nchini (cha viza) kwa mwenzangu, waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya kusini, na hata kwa kiongozi mashuhuri Nelson mandela,"

- Condoleeza Rice, akitetea muswada wa kuwaondoa viongozi wa chama tawala cha Afrika ya kusini, ANC, katika orodha ya vikundi vya kigaidi.

Mpaka sasa wanachama wa ANC huwa wanahojiwa kwa undani wanapotaka kuingia Marekani. Mwaka 2002, mwenyekiti wa ANC Tokyo Sexwale alinyimwa visa. Mwaka jana aliyekuwa balozi wa Afrika ya Kusini umoja wa Mataifa tangu 2002 mpaka 2006, pia alikataliwa visa ya kwenda kumuuguza nduguye mpaka baada ya huyo ndugu alipofariki dunia.

Sunday, April 20, 2008

MAHOJIANO NA THOMAS MAPFUMO


Thomas Mapfumo, mwanamuziki aliyehamasisha vita ya ukombozi wa Zimbabwe anadai kwamba Komredi Mugabe angeshakubali kuachia ngazi na kuwapa MDC uongozi wa serikali Zimbabwe. Anasema tatizo ni kwamba maswahiba wa Mugabe hawatamruhuzu mzee akubali kushindwa kwa vile wanahofia kushitakiwa kwa kukiuka haki za raia na serikali mpya ya MDC. ..

Mapfumo yuko ziarani Australia. Niliongea wiki iliyopita kuhusu muziki wake pamoja na siasa ya Zimbabwe.

Bofya hapo chini usikilize mahojiano hayo yaliyowezekana kwa hisani ya kipindi cha Afroworld ndani ya Radio Adelaide.MYKAL ROSE


Mahojiano na Mykal Rose ndani ya mrindimo wa dub - kwa hisani ya Abdalla Ezza.
Zawadi yako Rasta.