Friday, May 02, 2008

MANDELA BADO NI GAIDI MAREKANI

"Afrika ya kusini ni nchi ambayo tuna mahusiano mazuri nayo kwa sasa, ni jambo lanalotia aibu kwamba inanibidi kuondoa kikwazo cha pingamizi la kibali cha kuingia nchini (cha viza) kwa mwenzangu, waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya kusini, na hata kwa kiongozi mashuhuri Nelson mandela,"

- Condoleeza Rice, akitetea muswada wa kuwaondoa viongozi wa chama tawala cha Afrika ya kusini, ANC, katika orodha ya vikundi vya kigaidi.

Mpaka sasa wanachama wa ANC huwa wanahojiwa kwa undani wanapotaka kuingia Marekani. Mwaka 2002, mwenyekiti wa ANC Tokyo Sexwale alinyimwa visa. Mwaka jana aliyekuwa balozi wa Afrika ya Kusini umoja wa Mataifa tangu 2002 mpaka 2006, pia alikataliwa visa ya kwenda kumuuguza nduguye mpaka baada ya huyo ndugu alipofariki dunia.

No comments: