1
"May ur happiness increaselike fuel prices in TZ and your worries fall like number of votes to the opposition blocks in TZ, so that ur desires be fulfilled massively like kikwete's trips abroad. May your problems vanish like TANESCO's electricity. I wish u a happy and prosperous New year 2007."
1
Halafu tuendelee:
1
Mwezi wa 'kwanza' ndio umeshawadia katika kalenda ya kirumi. Mwezi uliobeba jina la mungu mmoja wa kirumi - Janus.
1
Janus, mungu wa hekaya za kirumi, mungu wa mabadiliko na vyanzo vipya, mungu aliyebeba funguo kama inavyoonyeshwa kwenye sanaa za kirumi.
1
Janus alikuwa na wajibu wa kufungua milango, viwambaza na vyanzo vingine vingine. Alikuwa na vichwa viwili, kimoja kinatazama mbele kimoja nyuma. Alikuwa na uwezo wa kulinda milango ya kuingilia na milango ya kutokea kwa wakati mmoja. Alikuwa na wajibu wa kuweka mizani ya matumaini ya wakati ujao kwa kuangalia matukio yaliyopita.
1
Nazungumzia mwezi wa januari nikijua kuwa ni mwaka mpya wa kirumi. Nifanyeje? Nilibahatika kuongea na babu yangu, Katego, (babu yake baba yangu) mwaka 1986 kabla hajaaga dunia. Nilimdodosa kuhusu kalenda za kikwetu.
Akanitajia miezi nane tu: Omuhangara; Omwiraguzu; Omwero gwilima; Omuhingo; Omworaguzu gw'echanda; Ekimezo; Kiswa; na Olubingo.
1
Pengine mwaka wa kikwetu ulikuwa na miezi nane tu au pengine ni kwa sababu ya uzee na ugonjwa wa usahaulifu, marehemu babu hakuweza kunitajia miezi mingine. Haidhuru, miezi ya kikwetu sijui jinsi ya kuipanga kwa utaratibu unaotakiwa au kuioanisha na misimu tunayoijua. Bora nizingumzie ninalojua.
1
Kwa kawaida wengi tunajipangia malengo binafsi ya kutimiza katika mwaka mpya. Wengine tunadhamiria kuwacha kuvuta tumbako, wengine kuwacha pombe, kupunguza vitambi, kubeba vyuma, kufanya mazoezi na kadhalika.
1
Malengo mengi huwa hayatekelezwi au yakitekelezwa basi kwa siku chache tu za mwezi wa januari. Malengi hayatekelezeki pengine kutokana na kwamba tunatumia kichwa kimoja tu cha Janus, kile kinachotazama mbele bila kutumia kichwa cha pili kinachoangalia tulikotoka.
1
Binafsi yangu lengo langu la kuwacha kuvuta tumbako nimeamua kuachana nalo vile kila mwaka nakata tamaa tarehe mbili ya Januari na kuendelea kulipuliza kama kawaida.
1
Basi hivi sasa nikiangalia nyuma na mbele najiwekea lengo linalowezekana. Lengo ambalo kila mmoja anaweza kutimiza:
1
Kutenda vitendo na kuacha kuahidi yasiyoyewezekana;
Kuwa mkweli kwa nafsi - kusema tunachoamini na kuamini tunachosema;
Kutenda haki na kudai haki;
Kutunza maadili na heshima;
Kukubali kusahihishwa tunapokosea.
Na kubwa zaidi kudumisha upendo kwani tunao uwezo wa kupenda - uwezo wa kubadili hali zetu kwa mawazo na vitendo chanya.
1
Bila kusahau kutoa shukrani kwa heri na fanaka zote zilizopita mwaka 2006, binafsi ikiwamo kumkaribisha mgeni mpya katika jamaa yangu, binti niliyebarikiwa wakati tukifungafunga mwaka - tarehe 22 desemba 2006. Jina lake nimemuita Nia.
1
Nawatakia heri ya mwaka mpya. 1