Monday, January 01, 2007

SALAMU ZA MWAKA MPYA (2)

Kwanza tushiriki ujumbe wa text nilioupata kwenye simu dakika chache zilizopita:
1
"May ur happiness increaselike fuel prices in TZ and your worries fall like number of votes to the opposition blocks in TZ, so that ur desires be fulfilled massively like kikwete's trips abroad. May your problems vanish like TANESCO's electricity. I wish u a happy and prosperous New year 2007."
1
Halafu tuendelee:
1
Mwezi wa 'kwanza' ndio umeshawadia katika kalenda ya kirumi. Mwezi uliobeba jina la mungu mmoja wa kirumi - Janus.
1
Janus, mungu wa hekaya za kirumi, mungu wa mabadiliko na vyanzo vipya, mungu aliyebeba funguo kama inavyoonyeshwa kwenye sanaa za kirumi.
1


Janus alikuwa na wajibu wa kufungua milango, viwambaza na vyanzo vingine vingine. Alikuwa na vichwa viwili, kimoja kinatazama mbele kimoja nyuma. Alikuwa na uwezo wa kulinda milango ya kuingilia na milango ya kutokea kwa wakati mmoja. Alikuwa na wajibu wa kuweka mizani ya matumaini ya wakati ujao kwa kuangalia matukio yaliyopita.
1
Nazungumzia mwezi wa januari nikijua kuwa ni mwaka mpya wa kirumi. Nifanyeje? Nilibahatika kuongea na babu yangu, Katego, (babu yake baba yangu) mwaka 1986 kabla hajaaga dunia. Nilimdodosa kuhusu kalenda za kikwetu.
Akanitajia miezi nane tu: Omuhangara; Omwiraguzu; Omwero gwilima; Omuhingo; Omworaguzu gw'echanda; Ekimezo; Kiswa; na Olubingo.
1
Pengine mwaka wa kikwetu ulikuwa na miezi nane tu au pengine ni kwa sababu ya uzee na ugonjwa wa usahaulifu, marehemu babu hakuweza kunitajia miezi mingine. Haidhuru, miezi ya kikwetu sijui jinsi ya kuipanga kwa utaratibu unaotakiwa au kuioanisha na misimu tunayoijua. Bora nizingumzie ninalojua.
1
Kwa kawaida wengi tunajipangia malengo binafsi ya kutimiza katika mwaka mpya. Wengine tunadhamiria kuwacha kuvuta tumbako, wengine kuwacha pombe, kupunguza vitambi, kubeba vyuma, kufanya mazoezi na kadhalika.
1
Malengo mengi huwa hayatekelezwi au yakitekelezwa basi kwa siku chache tu za mwezi wa januari. Malengi hayatekelezeki pengine kutokana na kwamba tunatumia kichwa kimoja tu cha Janus, kile kinachotazama mbele bila kutumia kichwa cha pili kinachoangalia tulikotoka.
1
Binafsi yangu lengo langu la kuwacha kuvuta tumbako nimeamua kuachana nalo vile kila mwaka nakata tamaa tarehe mbili ya Januari na kuendelea kulipuliza kama kawaida.
1
Basi hivi sasa nikiangalia nyuma na mbele najiwekea lengo linalowezekana. Lengo ambalo kila mmoja anaweza kutimiza:
1
Kutenda vitendo na kuacha kuahidi yasiyoyewezekana;
Kuwa mkweli kwa nafsi - kusema tunachoamini na kuamini tunachosema;
Kutenda haki na kudai haki;
Kutunza maadili na heshima;
Kukubali kusahihishwa tunapokosea.
Na kubwa zaidi kudumisha upendo kwani tunao uwezo wa kupenda - uwezo wa kubadili hali zetu kwa mawazo na vitendo chanya.
1
Bila kusahau kutoa shukrani kwa heri na fanaka zote zilizopita mwaka 2006, binafsi ikiwamo kumkaribisha mgeni mpya katika jamaa yangu, binti niliyebarikiwa wakati tukifungafunga mwaka - tarehe 22 desemba 2006. Jina lake nimemuita Nia.
1

Nawatakia heri ya mwaka mpya. 1

9 comments:

SIMON KITURURU said...

Hongera kwa kumpata jamaa mpya! Nimeipenda sana ujumbe uliopata kwenye text. Na nimependa na unanifikirisha ujumbe ulioundika!Tufurahie leo tuko hai!

Ndabuli said...

Natuma Hongera zangu kwako Mwandani kwa Kupata mgeni ambaye atakuwa mwenyeji mpaka hapo utakapomwambia sasa hama humu ndani...(heheheh)inabidi hapo kwa mgenu kutumia vichwa viwili.

mloyi said...

Omuhangara; Omwiraguzu; Omwero gwilima; Omuhingo; Omworaguzu gw'echanda; Ekimezo; Kiswa; na Olubingo.
Kumbe huku pia tunayomiezi kama wao! Vizuri tukiikumbika maana tunahesabu miungu ya kirumi siku zote na tunazidi kuwa masikini, na kushindwa kufikiria vizuri, kama huwa hatuiombi miungu au ni watu waliolaaniwa! Inabidi tuache kuifuata sana hii miungu na tutumie yetu ya asili.
Nini maana ya hiyo miezi uliyotuambia?

Anonymous said...

JT,

Tuwasiliane Sammy Davis! naona Pitopitonomi yupo Unyamwezini! Heri ya Mwaka Mpya!

BabaKulu

Anonymous said...

Kwanza napenda kukupongeza wewe na kaya yako kwa mgeni wa baraka. Pili kwa ujumbe mzito wa mwaka mpya. Tatu ni pongezi kwa blogu yako, ni hatari........Arip

mwandani said...

Arip, Babakulu nashukuru kwa kupitia kona hii. Heri izidi kuwafikia.

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
ndesanjo said...

Mlete mgeni aje hapa tuhangaike naye!
J. hongera sana kwa mgeni.

Pia kwa kuanzisha mwaka kwa somo la harakaharaka kuhusu miezi ya kalenda ya kirumi (inayochukuliwa pia kuwa kalenda ya kikristo ingawa inatumia imani na miungu ya kirumi kama zilivyo pia siku za juma). Masomo haya Tunga tunayahitaji zaidi na zaidi.

SaHaRa said...

Hongera sana kwa kupata mgeni mpya kwenye familia - kweli mmepata baraka nzuri ya mwaka. Nakutakia kila na kheri na mwaka huu mpya.