Saturday, March 10, 2007

MAHOTELLA QUEENS (Womadelaide 2007)

(Mahotella Queens - Womadelaide 2007)
1
Mahotella Queens ndio waliofungua dimba ya tumbuizo kwenye tamasha la 15 la Womadelaide. Baada tu ya baraka za ufunguzi, bila kuchelewa kikosi cha maajuza watatu kutoka Afrika ya kusini, Mahotella Queens walivamia jukwaa namba moja na kuporomosha vibao vyao vyote maarufu - pamoja na Kazet na Umuntu Ngumuntu. ilikuwa onyesho kabambe - kwa lugha ya wanamiziki wanasema walipiga "tight set".
12
Miye naona hii ni baraka kuwashuhudia maajuza hawa wakitumbuiza, kwani walisharitaya shughuli za muziki baada ya kupotelewa na wanamuziki wenzao watatu wakiwemo Mzee Mahlatini na West Nkosi. Naona ni baraka vile hawa madada wazee - Hilda Tloubatla, Nobesuthu Shawe Mbadu na Mildred Mangxola ndio historia ya muziki wa dansi wa Afrika ya kusini. Hawa ndio hasa waliokuwamo kwenye kuipika mbaqanga jive.
1
Na kama alivyokuwa akieleza Bibie Hilda Tloubatla akiwa jukwaani - bila kujituma, kukaza nia tena baada ya kukata tamaa na misiba pengine wasingelikuwapo ndani ya tamasha mwaka huu.

Shoo yao ilikuwa swafi sana - walikuwa na mpigaji gitaa zito, mpiga gitaa, mpiga ngoma (yaani "drums") na mpiga kinanda tu. Hata hivyo vibibi hivi vilitoa vichekesho na mawaidha kwa wanawake na wanaume.
1
Usia ambao pengine haukuwafikia vizuri watoto wadogo na vichwa maji wengine ni pale walipowaambia akina mama: "Mkitaka kuwa na afya na furaha, muweze kucheza kama sisi mpaka uzeeni, siri ni kujidamka alfajiri ya saa kumi, umpe mumeo staftahi, na akirejea kutoka kazini akute maakuli, basi mumeo mwenyewe atakuwa akiwahi kurudi nyumbani kila siku, na kama ana uwezo atakununulia chochote unachotaka". Ma-feminist walinung'unika na kauli.

3 comments:

Anonymous said...

Mwaka jana (2006)nilinunua cd ya The Best of the Mahotella Queens / The Township Idols. Hawa maajuza huwezi kuchoka kuwasikiliza halafu wamenimaliza sana na version yao ya Malaika kwa Kizulu.

Alipofariki Mzee Mahlatini Gazeti la Newsweek lilitangaza msiba wake. Mungu amrehemu na amani. Amen.

Vipi ulienda kumuona Griot Salif Keita wa damu ya Sundiata? Kama ulienda usikose kutuletea dondoo zake.

Masalaam,

F MtiMkubwa Tungaraza

Anonymous said...

Nakubaliana na MtiMkubwa. Kama umemuona mzee wa Yekeyeke, usiache kutumegea.

Chemi Che-Mponda said...

Nachowapendea waSouth Africa ni kuwa hawasahau utamaduni wao. Hata wakifanya kitu cha kisasa lazima waingize kitu cha utamaduni wao. Na sisi waBongo tusisahau utamaduni wetu tuache mambo ya kuiga West.

Mahotella Queens ni show safi sana ya kushuhudia.