Muasisi wa utengenezaji filamu barani Afrika, Sembene Ousmane amefariki dunia mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 84.
Sembene ndiye mwafrika wa kwanza kutengeneza filamu barani Afrika. Alikuwa mmojawapo wa wa waanzilishi wa tamasha la filamu Afrika, FESPACO. Alikuwa pia ni mtunzi wa vitabu. Kwa wale waliosoma somo la kiingereza wakiwa sekondari bila ya shaka walisoma pia kitabu cha God's Bits of Wood alichokiandika huyu mzee.
Binafsi nilivutiwa na kitabu hicho. Kadhalika nilivutiwa mno na filamu yake ya mwisho aliyoitengeneza, Moolaade. Mara baada ya kuiangalia nilieleza utamu wake kwenye blogu hii takriban miaka miwili hivi iliyopita.
Ameacha pengo lisilozibika - au pengine akiwa kama alama ya zama za filamu za mwanzo barani Afrika pia anafunga pazia la zama hizo - hasa kutokana na mabadiliko ya haraka yanayotokea katika utengenezaji na hadhira ya filamu za kiafrika barani hivi sasa.
3 comments:
Mwandani,
Habari hii imenitia huzuni.Nilivisoma vitabu vyake nikiwa shuleni na hata mtaani.Ni pengo kwa Afrika.Tutamkumbuka.
Tutamkumbuka Mzee!
Hi
Im trying to locate the picture you got of sembene ousmane. do you know who the photographer was or where I can get a copy of the picture?
Regards,
Torben
torben.krog@textuel-london.co.uk
Post a Comment