Friday, July 20, 2007

FIMBO YA MBALI INAUA NYOKA

Fimbo ya mbali inaua nyoka. Hizi zama za teknolojia za mitandao ya intaneti zinabadili mambo.
1
Jioni hii baada ya kazi nafungua barua pepe nakutana na tangazo la mkanda mfupi wa muziki wa Ras Nas. Na hivi ndiyo kwanza nimemaliza kuangalia na kusikiliza muziki wa Ras Nas - muwakilishi wa sanaa toka Tanzania.
1
Muziki timilifu kila upande. Anaanza kwa muziki mwororo wa miondoko laini ya rumba ila sebene lililofuata limeniamsha kitini. Ningekuwa na utaalamu wa youtube kama Kitururu ningepandisha filamu. Lakini si haba, kuna kiungo hapa ukibofya utafika kwenye hiyo filamu ya Ras Nas.
1

Halafu nasoma barua pepe nyingine nakutana na kiungo kingine cha muziki wa Tanzania: Chemundu & Mbega Arts. Japo hakuna filamu ya kikundi wala sauti kwenye tovuti - napata ujumbe kuwa sanaa Tanzania inatokota kisawasawa. Kwa maelezo yao:
1
Chemundu na Mbega Arts ni kikundi cha muziki wenye vionjo vya muziki jadi(asili) halisi wa Tanzania na pia kuchanganya na mitindo ya Kimataifa kama:pop,afro rhumba na afro jazz.
Mbega Arts ilianziswa na mwanamuziki maarufu Che Mundugwao " chem ". na kujumuisha wanamuziki na wasanii wa muziki wa jadi vijana wenye vipaji vya hali ya juu ,ambao wameshawahi kushiriki katika ziara na matamasha mbalimbali ya kitaifa(tamasha la sanaa Bagamoyo) na kimataifa katika nchi za Kenya,Sweden,Denmark,Finland,Uingereza.n.k
1
Hiyo isitoshe, ndani ya barua pepe nyingine nakuta jamaa wa Afropop Worldwide wanaitangaza Tanzania kinamna. Moja ya santuri wanazocheza katika juma la muziki wa Afrika (African Summer Dance Party) inatoka kwa bendi ya Tanzania FM Academia. FM wamewekwa bega kwa bega na Hugh Masekela na Ricardo Lemvo katika chaguo la wataalamu wa AfroPop.
1
Nimeshapata mshawasha, ngoja nielekee kwenye miziki mjini - kuna rege mitaa ya kati huko. Ijumaa hii silali ndani. Fimbo ya mbali ishanichapa.

2 comments:

Aliko said...

Mwandani
burudani zaidi unawezakuipata katika tovuti ya Sibelius Academy link ni http://www2.siba.fi/sibatv/index.php?id=54&la=en
pale utakutana naonyesho la HODI liloandiliwa na Dk chiwalala choreographer,director na washikaji wako wengine wa kijiwe cha hlki...pata burudani

Simon Kitururu said...

Umenifanya nistukie kuwa saa nyingine fimbo ya karibu unaizoea hata makali huyastukii:-)