Saturday, March 10, 2007

WOMADELAIDE 2007

(wazawa wa Adelaide - Kaurna - wakibariki tamasha)
1

Wikiendi hii tumerejea tena kwenye moja ya matamasha maarufu ya muziki wa kimadunia katika Australia - Womadelaide 2007. Mwaka huu tamasha hili ni la 15 hapa Adelaide na kwa mara ya kwanza kumekuwa na ratiba tofauti. Katika siku tatu za tamasha hili wanamuziki wote vinara wanatumbuiza mara moja tu. Haidhuru.
1
Bila kujali joto la kiangazi wapenzi wasiopungua 70 elfu wameshaanza kuburudika ndani ya viwanja vya Adelaide botanic park na wataburudika kwa siku tatu mfululizo mpaka nyasi kugeuka vumbi.
1
Pamoja na wanamuziki wa Kiafarika kama Femi Kuti (Nigeria), Salif Keita (Mali) na Mahotella Queens (Afrika ya Kusini) magwiji wengine kutoka pande zote za dunia kama akina Asha Bhosle (India); Kronos Quartet (US); Blue King Brown (Australia); Gotan Project (France / Argentina); Lior (Australia); Lunasa (Ireland); Emma Donovan Band (Australia); na Mariza (Portugal) watatumbuiza pia.
1
Kwa upande wangu mpaka hivi sasa nimeshahudhuria maonyesho ya bendi mbili za kutoka Afrika: Mahotella Queens na Femi Kuti and the Positive Force. Na bila ubishi wowote Mahotella Queens wamenisuuza moyo vilivyo.

(Bi mkubwa wa ki-Kaurna akisoma risala ya kubariki tamasha na kuwaenzi wenye nchi)
1
Kama ilivyo mila na desturi ya hapa Australia haianzi shughuli bila kutoa heshima kwa wazawa wa nchi hii wanaotambulika kama Ma-aborijino au Indigenous people ambao walikuwa 'hawatambuliki' kama binaadamu kamili kabla ya mwaka 1967.
1
Wazawa walianza kwa kutoa heshima ya ki-kaurna (inatamkwa ga-na). Mzee wa kabila (kama anavyoonekana pichani) alianza kusoma dua za kikwao akafuatiwa na vijana waliocheza ngoma ya kubariki tamasha. (juu kabisa pichani)

4 comments:

Simon Kitururu said...

Basi tu huko ni mbali.Lakini starehe umeipata huko. Labda hii uliyoifaidi ni anasa hii:-)

Mjengwa said...

Inafurahisha kuona picha na kusoma habari za mbali hivi

Anonymous said...

Mwandani,
Sio siri nakuonea wivu kwa kuwaona Mahotella Queens na Femi Kuti live mapema kabisa tunapoelekea kwenye majira ya joto.Mwaka jana nilinunua cd ya the best of mahotella queens na kwa kweli ningali nikiburudishwa nayo.

Simon Kitururu said...

Mwandani eeh!Kule kwangu mimi na Ndesanjo tumejadili jinsi unavyotunyima mashairi yako.Basi bwana, imebidi nikulalamikie.Sasa nifanyeje?