Sunday, August 19, 2007

Australia imefukuza watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe

Hatimaye serikali ya Australia imeitikia wito uliotolewa mwezi wa nne mwaka huu na gazeti la Zimdaily, wa kuwafukuza watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe ambao wanasoma ughaibuni kama njia mojawapo ya kuwaadhibu viongozi hao.

Adhabu hiyo imetolewa wakati viongozi wa SADC huko Zamnbia wakiwa wakikubaliana kwamba hali ya Zimbabwe sio mbaya kama wamagharibi wanavyodai. Maamuzi ya Australia na yale ya viongozi wa SADC yanafuatana kama vile mabodia wanavyotupiana masumbwi moja baada ya jengine.

Wakati zoezi la kuwataja kwa majina, pamoja na anwani za wanapoishi watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe lilipozuka mwezi wa nne mwaka huu - zoezi liliondaliwa na gazeti la Zimdaily msimamo wangu ulikuwa: sioni haki ya binaadamu mmoja kushinikizwa kwa kutumia binadamu mwingine. Kwamba ikiwa baba yangu ana makosa fulani basi na mimi nihukumiwe kwa makosa yale.

Nilitundika maoni pale kwa Jikomboe, wengine walikuwa na mawazo tofauti. Nikichukulia mfano, kama mimi ningekuwa mmojawapo wa watoto wale, mwenye mawazo tofauti na baba yangu, pengine nimetumia skolashipu iliyoangalia uwezo wangu wa kimasomo, na ninafanya vizuri tu shuleni, halafu nizuiwe kuendelea na masomo kwa sababu baba yangu anafanya kazi serikalini… Haki yangu ya kuishi kama mtu huru itakuwa iko wapi.

Ninaelewa haki ya taifa lolote kuwa na uamuzi ni nani anayeweza kuishi katika mipaka yake nabaki na tatizo la kuelewa dhana ya haki za kibinadamu katika hili.

12 comments:

Simon Kitururu said...

Swala linanitatiza hili.Hali ya Zimbabwe nishai.Halafu eti wa upinzani bado wanashindwa kukubaliana kujiunga kutokana na ukabila!

NDABULI said...

Hapo pagumu hapo!

Anonymous said...

Nina mawazo sawa na yako Tunga, kwamba tusije kufanya kama tunavyoona kwenye biblia ambapo watoto (hadi vizazi sijui vya ngapi) wanalaaniwa kwa makosa ya wazazi wao. Aliyekula tunda ni Eva, tunaambiwa eti laana ikatolewa kwa wanawake wote milele. Adamu naye akakosa, kama kitabu kile kinavyosema, laana ikatolewa kwa wanaume wote. Naambiwa eti hata sisi weusi tuna laana ya mtoto wa Nuhu aliyemchungulia babake....habari hizi zinachekesha kweli.

Tuache hadithi, turudi kwenye Australia. Watoto hawa ni watu wazima. Huenda hawakubaliana hata kidogo na mwenendo wa wazazi wao. Zaidi ya hilo, wana haki ya kibinadamu ya kusoma popote pale iwapo wana uwezo na wametimiza masharti. Sijawahi kusikia sharti kuwa huwezi kusoma chuo fulani kama baba yako anafanya kazi kwenye serikali ya Zimbabwe. Pengine watoto waliokuwa na mawazo tofauti na wazazi wao, hivi sasa wataanza kuwa upande wao kwa kuona kuwa wananyanyaswa bila sababu za msingi.

Hector Mongi said...

Nami naungana na Joe pamoja na Ndesanjo kulaani hatua hii. Tuna mifano mingi katika nchi zetu ambapo mtoto wa kiongozi wa chama anatofautiana kabisa na baba yake kiitikadi na kuwa mfuasi wa chama kingine.

Bob Sankofa said...

Tulishawahi kulaani hili huko nyuma. BAdo ninalaani, Zimbabwe na Australia wote ni wahalifu na tutawapeleka kwa People's court kwa hili

Anonymous said...

Tungaraza,msimamo wako huo,na pia wa wengine waliotoa mani kwamba:"sioni haki ya binaadamu mmoja kushinikizwa kwa kutumia binadamu mwingine. Kwamba ikiwa baba yangu ana makosa fulani basi na mimi nihukumiwe kwa makosa yale".Ni msimamo ambao nchi nyingi za magharibi wanaoutegemea kwenye mambo ya malipo kwa makosa na maovu mababu zao waliyoyafanya kwenye biashara ya utumwa na pia kwenye ukoloni na ukatili wake.Kufuatiliana na msimamo huo ingetubidi sisi waafrika,tulioteseka sana chini ya ukoloni na utumwa,tuwasamehe waliotukosea na kuwapenda kwa roho yote. Lakini inaelekea wengi sisi waafrika hatutaki au hatuwezi kusamehe mambo hayo. Hii inaonyeshwa na hatua ya viongozi wa SADC,na waafrika wengi,kumshangilia Mugabe kwa hatua zake;ultimately wengi wanamuunga mkono Mugabe kwa kua ana "mabavu" au ni mwanaume halisi kwani "amewadindia" hao wazungu.
Kama tungefuata msimamo wako kwa kweli ingetubidi tuwasamehe hao wazungu,ingawaje utajiri wao na mali yao (mashamba etc) huko Zimbabwe ulipatikana kwa madhambi na ubabe wa "mababu zao".
Swali langu ni hili: mbona tunakua wazito kuwasamehe ndugu zetu waliotukosea, lakini ni wepesi kulaani?
Pia tukisema kwamba tunaishi in a politicaly "neutral" world tutakua tunadanganyana. Kwahiyo kwa akili za binadamu Australia wana “haki” ya kuwafukuza hao wanafunzi kama vile Mugabe alivyowafukuza ndugu zao hao Australia.
Ulivyosema kwamba “Maamuzi ya Australia na yale ya viongozi wa SADC yanafuatana kama vile mabondia wanavyotupiana masumbwi moja baada ya jengine” ni kweli. Swali la kumalizia ni hili: wakipigana tembo anaye umia ni nani?
K

Anonymous said...

WHY AFRICA MUST SUPPORT ZIMBABWE
By George Nyan

There is nothing more exhilarating and empowering than a change of consciousness. The biggest reason for the lack of development in Africa has been the poor leadership on the continent and Western economic interest. The case of Zimbabwe is making waves right now because of the awakening of the conscience of the leadership.

Regardless of what one thinks of Mugabe what happens to Zimbabwe will set the tone for Namibia, South Africa, and Mozambique when it comes to Land reform and redistribution of resources from the white minority to the black majority.

The international assault against Zimbabwe for Mugabe returning land occupied by white farmers to indigenous Africans is unjustified because the real victims have been the Zimbabwean people.

No emphasis is made of the billions owed to Zimbabwe by Britain. Independence means that Zimbabwe has the right to decide what to do with her resources since Britain did not honor the terms and conditions of the Lancaster agreements.


The modus operandi now on the continent is that African governments must compensate white farmers for "their" land, but no mention whatsoever of compensating Africans for the stolen land, resources, and national treasures. Families have been displaced, communities were turned into laborer camps, and the fruit of the land is still being enjoyed by the minority whites.

Land and resources in Africa were not bought or negotiated for, they was taken at gun point and if the original inhabitants want them back now they have to pay for them. Any mention of reparations by an African leader is met with hash objection and criticism, he will be vilified and seen as a militant.

The rationale for extending colonialism and apartheid in Africa was because Europeans argued that Blacks were not intelligent and capable of handling a modern political state. Any government that tried to serve her interest against the interest of the West was sabotaged and replace with a dictator that maintained Western economic interest.

Why did we not see this kind of backlash against the regimes of Mobutu, Eyedama, Biya, Boigny, and others, instead the West was silent just like they were with Mugabe when he protected their interest but turned on him when he woke up and decided to collect money owned to Zimbabwe by Britain.

The support of African dictators by Western power serves two points. First, it maintains their dominance and control of Africa’s resources. The West will not make the mistake they made from 1820 to 1885 when they decided to trade fairly with Africa after the abolition of slavery.

Rubber, cotton, palm oil, and ivory that used to be taken for nothing had to be bought at market prices, this was crippling the European economy while Africa experienced a period of economic resurgence and immense wealth distribution.

When they could not afford to buy the raw materials needed to fuel the industrial revolution, they simply decided to invade and colonize the continent. Secondly, these failed African states perpetuate the stereotype of the African being inferior and legitimize the meddling into African affairs by non- Africans.

We need to support Zimbabwe because the success of her means that an African state can survive and function without the aid or interference of the West. This is important in dispelling stereotypes and popularly held by racist beliefs about the inferiority of the Black man and his inability to organize and govern himself (with disregard to history).


Success will also mean that other African regimes maintaining Western interest at the expense of their people will not be tolerated, lessons learned and policy implemented in Zimbabwe could be duplicated in other countries that are facing similar situations. Most of all, the intangible feeling of pride and brotherhood will flow throughout the continent.

Progress has been made in Zimbabwe since the assault and economic sabotage began from Britain and her allies. Debts to IMF, World Bank, and commonwealth have been paid off, new tractors arrived in time before the raining season, construction and economic policies are in place.

It is important for everyone to have realistic expectations about how soon we will begin to see changes from policies that have been implemented. Failure is not an option at this point and demonizing Mugabe will not help the situation, we need to do whatever it takes to support the Zimbabwean people during this period of transformation. In the words of Sekou Toure of Guinea who was vilified after defying the French ‘the Guinean people preferred poverty in freedom than to riches in slavery’.

George Nyan is a Counsultant with Africa Political & Economic Strategic Center and writes from Nigeria

Anonymous said...

Hiyo article hapo juu inatusomesha vizuri sana. Ili kumaliza matatizo ya Zimbabwe, swala la ardhi kutumiwa na WOTE(kwa sasa ni mali ya wazungu wachache tu)laim litatuliwe. Mugab, 83, i ishu kwa sasa, kwani miaka 100 badae kama tatizo hilo halijshughulikiwa tutakuwa hapahapa, na kina Mugabe wengine ambao hawajzaliwa!

Anonymous said...

Hiyo article hapo juu inatusomesha vizuri sana. Ili kumaliza matatizo ya Zimbabwe, swala la ardhi kutumiwa na WOTE(kwa sasa ni mali ya wazungu wachache tu)lazima litatuliwe. Mugabe, 83, si ishu kwa sasa, kwani miaka 100 baadae kama tatizo hilo halijashughulikiwa tutakuwa hapahapa, na kina Mugabe wengine ambao hawajzaliwa.(Nimerudia kurekebisha spellings)

Anonymous said...

Nia na madhumuni ya serikali ya Zimbabwe si nzuri, ingawa uamuzi huu mimi binafsi nimeupenda. Kwanini watoto hawa wa vigogo wasisome Zimbabwe? Wao wanasoma australia, jee na wale wa wazimbabwe wa mchafukoge wanasoma zimbabwe au hawasomi kabisa. Pumbafu, fukuzilia mbali.

Anonymous said...

Thanks George Nyan, you have really put this issue in the right perspective. Alot of our people have been blind folded by the Westen media who blame Zimbabwe leaders while Britain is to blame. Alot of people think what they see in the tv is what it is. In the politics and economics of today you must go a bit deeper to get the real thing.

THANKS GEORGE!

Anonymous said...

Who knows where to download XRumer 5.0 Palladium?
Help, please. All recommend this program to effectively advertise on the Internet, this is the best program!