Saturday, March 10, 2007

FEMI KUTI AND THE POSITIVE FORCE (Womadelaide 2007)

(Femi Kuti akitumbuiza Ijumaa usiku 9-3-07)

Shoo nyingine ya kutoka Afrika hapa katika Tamasha ni ile ya mwanamuziki Femi Kuti wa Nigeria. Bila ya shaka hii ilikuwa ndiyo bendi kubwa kupita zote usiku wa Ijumaa. Kulikwa kuna waimbaji, wapiga midomo ya bata ya aina zote (trumpets, alto na tenor sax, trombone, nk.) wapiga ngoma wawili, wanenguaji watatu, wapiga magitaa wawili, na mpiga gitaa zito, mpiga vinanda… pamoja na Femi mwenyewe ambaye anapuliza midomo ya bata ya aina mbili pamoja na kupiga kinanda na kuimba, kuunguruma na kufoka.
1
Onyesho lake lilikuwa ni nguvu na sauti kubwa mno. Ilikuwa kama vile amefunga vipaza sauti vya shoo za rock 'n' roll au heavy metal. Niliwaona wazee wachache wakihama mistari ya mbele huku wakiziba masikio.

Shoo ya femi ilikuwa sawa na kumsikiliza baba yake - Fela. Kulikwa na mseto wa Afro-beat na jazz ya haraka haraka. Alitoa maneno makali dhidi ya Obasanjo na viongozi wengine wa Kiafrika. Kadhalika aliwasuta waafrika waliokuwapo uwanjani, na kuwahimiza kufanya kweli. Ukiopndoa kibao cha Do Your Best na Beng Beng Beng, vibao vyote vilikuwa ni vya kisiasa.
1
Huyu bwana Femi alitoa sare na ma-Aborigine katika kupuliza sax. Ma-aborigines wanajulikana kwa mtindo wao wa kupiga digderidoo (aina ya filimbi kubwa yenye sauti nzito) huku wakitumia circular breathing. Femi alionyesha umahiri huo kwa kupuliza mlio mmoja wa sax kwa dakika kama mbili na nusu bila kukata.

Pamoja na kupenda sana kuangalia wanenguaji wa kike, mtindo wa wananguaji wa Femi wa kuwapa mgongo watazamaji huku kitambaa (au kijichupi) kikiwa kinavuka na kuonyesha msamba mara kwa mara kidogo kilinifanya nifadhaike. Vinginevyo ile dansi yao maarufu kana kwamba wanafanya mapenzi na mwanamume nadhani iliwavutia wengi pamoja na wapiga picha waliojazana upande wa wanenguaji.

Baada ya onyesho nilimkuta Msenegali mmoja anayepiga muziki hapa Adelaide, Lamin, akibishana na wazungu juu ya Femi. Wazungu wanadai waliupenda sana ule muziki kwani 'the whole stage was busy, the man's got energy, oooh!" Msenegali alikuwa anadai kuwa hakuweza kuucheza mziki ule kwa filingi.

2 comments:

Anonymous said...

Tunga,
maneno haya. Femi nampenda, ila baba yake ndio hakuna mfano. Halafu yule mdogo wake Femi ndio hazimo kabisa kama baba yake. Sijui kama umewahi kumuona. Kila kitu kama baba yake: kucheza, maneno makala ya kisiasa, ukorofi, ukaidi, n.k.

Uliposema alipiga nyimbo zake mbili za zamani ulinikumbusha tabia moja ya Fela Kuti. Fela alikuwa akisharekodi wimbo basi usitegemee kumuona akiuimba kwenye onyesha lake. Alikuwa akisema kuwa anataka watu waone alivyopiga hatua. Yaani kama wimbo alirekodi mwaka juzi, kwanini akifanya onyesho leo aupige huo badala ya kupiga nyimbo mpya alizotunga wiki jana? Basi alikuwa harudii wimbo akishaurekodi.

Tupe zaidi.

Anonymous said...

Aiseh Mr Tungaraza, asante sana kwa hii post - imenifurahisha sana, to the point of feeling as if i was seeing the whole thing "laivu".
Ubarikiwe