Tuesday, November 06, 2007
RISING VOICES
Unaweza ukapata dola 5000 zitakazokuwezesha kufundisha wengine. Unachotakiwa kufanya ni kutuma maombi kwa jamaa wa raising voices. Mstari mfu ni novemba 30, 2007.
Fanya utume. Bofya hapa kwa maelezo zaidi. Fomu za maombi zipo mwishoni mwishoni mwa ukurasa.
Mtazamo mbadala: Shivji ahoji tuzo ya Mo Ibrahim
"Mo Ibrahim’s prize for a retired African president which was awarded to Joachim Chissano of Mozambique was in my view an insult to the African people." Issa Shivji raises a number of questions around the award such as how and what is "good governance" and why is it only applied to Africa? And most importantly "for which and whose democracy they are getting a prize".
According to the media, "Mo Ibrahim, a Sudanese-born telecommunications entrepreneur, established the prize as a way of encouraging good governance in a continent blighted by corruption and a frequently loose adherence to democratic principles." Not a word is mentioned about the living conditions of the people of the Sudan from where Mr. Ibrahim hails…..
But, isn’t this prize also a sign of the political retrogression in Africa? The idea of a President voluntarily stepping down is now so novel in the face of leaders such as Museveni and Mugabe that Chissano indeed stands out. Compared to Robert Mugabe and Thabo Mbeki, and their megalomanic policies, Chissano does look good.
Sunday, September 23, 2007
TOA MAONI - PENDEKEZA BLOGU BORA AFRIKA
Dondoo za katiba ziko ndani ya blogu ya JUMUWATA, hivyo maoni ya wengi yanahitajika ili isije ikawa ni watu wachache wameamua tunaenda wapi.
Mchango wa wanablogu wenye blogu na wasio na blogu unahitajika ilikuwa na kitu kikamilifu kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine.
Mapendekezo ya blogu bora Afrika yanafikia mstari mfu tarehe 30 mwezi wa Tisa.
Kama kuna blogu inayoandikwa na Mwafrika ambayo inakukuna moyo fanya uipendekeze ndani ya ukurasa huu.
Hapa chini ni maelezo ya kimombo:
Best of the Blogs: Deutsche Welle
Nominate your favorite blogs today! You're a blogger? You know a good blog? You like blogs, videoblogs and podcasts and want to share your favorites with the world?
Thursday, September 13, 2007
Cha kushangaza, hivi hawakuweza kupata mrembo mkubwa kwa umri kidogo, halafu akasitiri kidogo kifua chake, ambaye wasingempaka masizi kumfanya awe mweusi tii. Nijuavyo Marekani kuna weusi tii kwa wingi.
Sina hakika mlengwa wa biashara hii ni nani, japo tangazo limezua gumzo.
Tuesday, August 28, 2007
MWANZO WA MWISHO WA SIASA ZA RAFU?
"Inashangaza Zitto ambaye amepewa ‘red card’ bungeni kushabikiwa na idadi kubwa ya Watanzania wakiwemo wana CCM ambao walikwenda Jangwani kumlaki na kumsikiliza wakati akitokea Dodoma, ni lazima tukisafishe chama ili wapinzani wasije kutupiku,"
Sunday, August 19, 2007
Australia imefukuza watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe
Adhabu hiyo imetolewa wakati viongozi wa SADC huko Zamnbia wakiwa wakikubaliana kwamba hali ya Zimbabwe sio mbaya kama wamagharibi wanavyodai. Maamuzi ya Australia na yale ya viongozi wa SADC yanafuatana kama vile mabodia wanavyotupiana masumbwi moja baada ya jengine.
Wakati zoezi la kuwataja kwa majina, pamoja na anwani za wanapoishi watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe lilipozuka mwezi wa nne mwaka huu - zoezi liliondaliwa na gazeti la Zimdaily msimamo wangu ulikuwa: sioni haki ya binaadamu mmoja kushinikizwa kwa kutumia binadamu mwingine. Kwamba ikiwa baba yangu ana makosa fulani basi na mimi nihukumiwe kwa makosa yale.
Nilitundika maoni pale kwa Jikomboe, wengine walikuwa na mawazo tofauti. Nikichukulia mfano, kama mimi ningekuwa mmojawapo wa watoto wale, mwenye mawazo tofauti na baba yangu, pengine nimetumia skolashipu iliyoangalia uwezo wangu wa kimasomo, na ninafanya vizuri tu shuleni, halafu nizuiwe kuendelea na masomo kwa sababu baba yangu anafanya kazi serikalini… Haki yangu ya kuishi kama mtu huru itakuwa iko wapi.
Ninaelewa haki ya taifa lolote kuwa na uamuzi ni nani anayeweza kuishi katika mipaka yake nabaki na tatizo la kuelewa dhana ya haki za kibinadamu katika hili.
Friday, July 20, 2007
FIMBO YA MBALI INAUA NYOKA
Jioni hii baada ya kazi nafungua barua pepe nakutana na tangazo la mkanda mfupi wa muziki wa Ras Nas. Na hivi ndiyo kwanza nimemaliza kuangalia na kusikiliza muziki wa Ras Nas - muwakilishi wa sanaa toka Tanzania.
1
1
Chemundu na Mbega Arts ni kikundi cha muziki wenye vionjo vya muziki jadi(asili) halisi wa Tanzania na pia kuchanganya na mitindo ya Kimataifa kama:pop,afro rhumba na afro jazz.
Mbega Arts ilianziswa na mwanamuziki maarufu Che Mundugwao " chem ". na kujumuisha wanamuziki na wasanii wa muziki wa jadi vijana wenye vipaji vya hali ya juu ,ambao wameshawahi kushiriki katika ziara na matamasha mbalimbali ya kitaifa(tamasha la sanaa Bagamoyo) na kimataifa katika nchi za Kenya,Sweden,Denmark,Finland,Uingereza.n.k
Nimeshapata mshawasha, ngoja nielekee kwenye miziki mjini - kuna rege mitaa ya kati huko. Ijumaa hii silali ndani. Fimbo ya mbali ishanichapa.
Tuesday, June 26, 2007
Nyerere Press Conference - 14 March 1995
"Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption,"
"This would not only lead to collapse of the now-sensitive 30-year-old union between the twin-islands of Zanzibar and Pemba and Tanzania mainland, but would also plunge the country into chaos," (talking about condoning religious differences and tribalism)
Monday, June 11, 2007
SEMBENE OUSMANE AFARIKI DUNIA
Friday, June 01, 2007
MRADI WA KUIMARISHA SHUGHULI ZA BLOGU
1
Kama akina Maggid kama wanavyoonekana pichani hapo juu.
Hata hivyo haidhuru kama utapatikana msaada zaidi kidogo ili kurahisisha mambo.
Endelea hapo chini, kama unaweza kufuatilia kabla ya tarehe 15 juni fanya harahara.
Application Deadline: June 15, 2007
Rising Voices, the outreach arm of Global Voices, is now accepting project proposals for the first round of microgrant funding of up to $5,000 for new media outreach projects. Ideal applicants will present innovative and detailed proposals to teach citizen media techniques to communities that are poorly positioned to discover and take advantage of tools like blogging, video-blogging, and podcasting on their own.
Purchasing an affordable digital video camera and teaching a group of rural students how to produce an ongoing video-blog documentary about the lives of their grandparents.- Organizing a regular workshop on blogging and photography at a local orphanage. Portions of the budget could be used on cheap digital cameras and internet cafe costs so that participants could describe their local neighborhoods to a global audience with text and photos.
- Working with a local NGO or social entrepreneur so that their challenges, successes, and stories are told to a global audience.
- Translating our new media curriculum to an indigenous language, like Quechua or Wolof, that is currently not represented in the blogosphere or "podosphere." Then use the learning modules to encourage bloggers to write in those languages.
The sky is the limit, but unfortunately funding is not. Rising Voices outreach grants will range from $1,000 to $5,000. Please be as thoughtful, specific, and realistic as possible when drafting your budgets.
Feel free to ask questions in the comments section below or by sending an email to
outreach@globalvoicesonline.org
Monday, May 07, 2007
CHEMA HAKIDUMU
Ungawa na hamu kukingojeleza
Saa ikitimu kitakuteleza
Chema wangu babu Kibwana Bashee
Alojipa tabu kwamba anilee
Illahi Wahabu mara amtwee
Hizo beti mbili nilizikariri zamani kutoka kwenye kitabu cha Abdilatif Abdala "Sauti ya Dhiki". Na kama ninavyozikumbuka zimekuwa zinanizinga mawazoni kwa masiku kadhaa sasa.
Nimeingiwa na machungu na woga. Uwezo wangu wa kufikiri au kutatua matatizo yaliyonifika umeniponyoka. Maisha yamenikumbusha uwanaadamu wangu. Kinachonisukuma ni ule moyo wa stahamali tu. Na ninaomba nijaaliwe stahamali zaidi.
Kitambo kidogo kilichopita Mwenyezi Mungu alimtwaa kipenzi Mama yangu Mkubwa, Kadala. Marehemu Kadala nilikuwa naye karibu sana wakati wa utoto wangu.
Naam, ndio maisha. Na hapa nilipo maisha mengine yanaenda kwa kasi ya mwendo wa radi. Nakimbiakimbia, ninachakurachakura kama kuku kutwa nzima. Kukicha naanza tena kama jana. Ndio maisha.
Basi naona bora kukawia kuliko kuiwacha safari. Tupo wote safarini japo tunaonana kwa nadra bloguni. Mambo yakisawazika bila ya shaka nitaongeza kasi na huku kwenye mitandao pia.
Haidhuru. Kule kwenye kurasa za Global Voices baada ya muda kama mwezi hivi kuna muhtasari wa blogu za kiswahili uliopandishwa leo. Tafadhali tupa jicho na huko pia. Bila kusahau kuperuzi kidogo kwenye ukurasa wa Reuters Tanzania.
Saturday, March 10, 2007
WOMADELAIDE 2007
1
Wikiendi hii tumerejea tena kwenye moja ya matamasha maarufu ya muziki wa kimadunia katika Australia - Womadelaide 2007. Mwaka huu tamasha hili ni la 15 hapa Adelaide na kwa mara ya kwanza kumekuwa na ratiba tofauti. Katika siku tatu za tamasha hili wanamuziki wote vinara wanatumbuiza mara moja tu. Haidhuru.
1
Bila kujali joto la kiangazi wapenzi wasiopungua 70 elfu wameshaanza kuburudika ndani ya viwanja vya Adelaide botanic park na wataburudika kwa siku tatu mfululizo mpaka nyasi kugeuka vumbi.
1
Pamoja na wanamuziki wa Kiafarika kama Femi Kuti (Nigeria), Salif Keita (Mali) na Mahotella Queens (Afrika ya Kusini) magwiji wengine kutoka pande zote za dunia kama akina Asha Bhosle (India); Kronos Quartet (US); Blue King Brown (Australia); Gotan Project (France / Argentina); Lior (Australia); Lunasa (Ireland); Emma Donovan Band (Australia); na Mariza (Portugal) watatumbuiza pia.
1
Kwa upande wangu mpaka hivi sasa nimeshahudhuria maonyesho ya bendi mbili za kutoka Afrika: Mahotella Queens na Femi Kuti and the Positive Force. Na bila ubishi wowote Mahotella Queens wamenisuuza moyo vilivyo.
(Bi mkubwa wa ki-Kaurna akisoma risala ya kubariki tamasha na kuwaenzi wenye nchi)
1
Kama ilivyo mila na desturi ya hapa Australia haianzi shughuli bila kutoa heshima kwa wazawa wa nchi hii wanaotambulika kama Ma-aborijino au Indigenous people ambao walikuwa 'hawatambuliki' kama binaadamu kamili kabla ya mwaka 1967.
Wazawa walianza kwa kutoa heshima ya ki-kaurna (inatamkwa ga-na). Mzee wa kabila (kama anavyoonekana pichani) alianza kusoma dua za kikwao akafuatiwa na vijana waliocheza ngoma ya kubariki tamasha. (juu kabisa pichani)
MAHOTELLA QUEENS (Womadelaide 2007)
1
Miye naona hii ni baraka kuwashuhudia maajuza hawa wakitumbuiza, kwani walisharitaya shughuli za muziki baada ya kupotelewa na wanamuziki wenzao watatu wakiwemo Mzee Mahlatini na West Nkosi. Naona ni baraka vile hawa madada wazee - Hilda Tloubatla, Nobesuthu Shawe Mbadu na Mildred Mangxola ndio historia ya muziki wa dansi wa Afrika ya kusini. Hawa ndio hasa waliokuwamo kwenye kuipika mbaqanga jive.
FEMI KUTI AND THE POSITIVE FORCE (Womadelaide 2007)
Wednesday, February 14, 2007
KWA WAPENDANAO
Kuadhimisha siku ya wapendanao, ambayo ni leo, kwa wale mnaoweza sanaa ya kuandika mashairi ya mapenzi, , mnashauriwa kushiriki kwenye shindano la mashairi ya siku ya wapendanao la sauti za dunia. Hata kama hutaki kushiriki kuandika - suuza moyo wako hapa kwa kuperuzi sehemu ya maoni palipojaa mashairi yaliyokwishatumwa.
Monday, January 01, 2007
SALAMU ZA MWAKA MPYA (2)
1
"May ur happiness increaselike fuel prices in TZ and your worries fall like number of votes to the opposition blocks in TZ, so that ur desires be fulfilled massively like kikwete's trips abroad. May your problems vanish like TANESCO's electricity. I wish u a happy and prosperous New year 2007."
1
Halafu tuendelee:
1
Mwezi wa 'kwanza' ndio umeshawadia katika kalenda ya kirumi. Mwezi uliobeba jina la mungu mmoja wa kirumi - Janus.
1
Janus, mungu wa hekaya za kirumi, mungu wa mabadiliko na vyanzo vipya, mungu aliyebeba funguo kama inavyoonyeshwa kwenye sanaa za kirumi.
1
Janus alikuwa na wajibu wa kufungua milango, viwambaza na vyanzo vingine vingine. Alikuwa na vichwa viwili, kimoja kinatazama mbele kimoja nyuma. Alikuwa na uwezo wa kulinda milango ya kuingilia na milango ya kutokea kwa wakati mmoja. Alikuwa na wajibu wa kuweka mizani ya matumaini ya wakati ujao kwa kuangalia matukio yaliyopita.
1
Nazungumzia mwezi wa januari nikijua kuwa ni mwaka mpya wa kirumi. Nifanyeje? Nilibahatika kuongea na babu yangu, Katego, (babu yake baba yangu) mwaka 1986 kabla hajaaga dunia. Nilimdodosa kuhusu kalenda za kikwetu.
Akanitajia miezi nane tu: Omuhangara; Omwiraguzu; Omwero gwilima; Omuhingo; Omworaguzu gw'echanda; Ekimezo; Kiswa; na Olubingo.
1
Pengine mwaka wa kikwetu ulikuwa na miezi nane tu au pengine ni kwa sababu ya uzee na ugonjwa wa usahaulifu, marehemu babu hakuweza kunitajia miezi mingine. Haidhuru, miezi ya kikwetu sijui jinsi ya kuipanga kwa utaratibu unaotakiwa au kuioanisha na misimu tunayoijua. Bora nizingumzie ninalojua.
1
Kwa kawaida wengi tunajipangia malengo binafsi ya kutimiza katika mwaka mpya. Wengine tunadhamiria kuwacha kuvuta tumbako, wengine kuwacha pombe, kupunguza vitambi, kubeba vyuma, kufanya mazoezi na kadhalika.
1
Malengo mengi huwa hayatekelezwi au yakitekelezwa basi kwa siku chache tu za mwezi wa januari. Malengi hayatekelezeki pengine kutokana na kwamba tunatumia kichwa kimoja tu cha Janus, kile kinachotazama mbele bila kutumia kichwa cha pili kinachoangalia tulikotoka.
1
Binafsi yangu lengo langu la kuwacha kuvuta tumbako nimeamua kuachana nalo vile kila mwaka nakata tamaa tarehe mbili ya Januari na kuendelea kulipuliza kama kawaida.
1
Basi hivi sasa nikiangalia nyuma na mbele najiwekea lengo linalowezekana. Lengo ambalo kila mmoja anaweza kutimiza:
1
Kutenda vitendo na kuacha kuahidi yasiyoyewezekana;
Kuwa mkweli kwa nafsi - kusema tunachoamini na kuamini tunachosema;
Kutenda haki na kudai haki;
Kutunza maadili na heshima;
Kukubali kusahihishwa tunapokosea.
Na kubwa zaidi kudumisha upendo kwani tunao uwezo wa kupenda - uwezo wa kubadili hali zetu kwa mawazo na vitendo chanya.
1
Bila kusahau kutoa shukrani kwa heri na fanaka zote zilizopita mwaka 2006, binafsi ikiwamo kumkaribisha mgeni mpya katika jamaa yangu, binti niliyebarikiwa wakati tukifungafunga mwaka - tarehe 22 desemba 2006. Jina lake nimemuita Nia.
1
Nawatakia heri ya mwaka mpya. 1
SALAMU ZA MWAKA MPYA (1)
1
Ujumbe huo makini nimekutana nao kwenye barua pepe za kimalumbano mtandaoni. Rafiki yangu Majaliwa katutakia heri ya mwaka mpya huku akitathmini ufanisi wa serikali ya awamu ya nne hususan kuhusiana na suala la umeme kama ilivyoandikwa kwenye magazeti hivi karibuni:
1
Kwa kweli Tanesco/umeme umekua dosari kubwa sana kwa JK's first year as president . Electricity generation technology is old and the supply and retailing of energy are now over 100 years old kwa hiyo hakuna sababu yoyote inayotulazimisha sisi wa TZ kuteseka kiasi hiki (by the way, when I say this I don't mean just in terms of lost opportunities/inconvenience from rationing but the millions of dollars-probably borrowed dollars - which are being wasted could be better spent in education, health and other essential services including road maintenance and water supplies).
1
What TZ needs is an independent regulator to forecast demand/supply and inform the market of future investment opportunities. This will mean some genuine reform to current arrangement for electricity generation and supply in Tanzania. Without genuine reform and long term plans aimed at meeting the growth in demand for electricity we will keep falling back on these short-term and expensive emergency fall-back/stopgap measures kila wakati ukame or plant breakdowns occur.
1
Na Hiyo TANESCO as it stands appears to be a wounded beast being used by different players to enhance their standing in the community as they are reliant on the 15 million plus in subsidies from the government (CCM).
1
Nauliza jamani kama hao CCM wameshindwa ku-ensure that the company runs effectively and efficiently in the 30+ years that they have had a monopoly on directing board/managerial appointments what makes them think that they can start now?
1
While there are good reasons for government ownership for key strategic assets for the benefit of the country it is not clear kwamba TANESCO is actually benefiting from this.
1
A good example of a possible way forward is our next door neighbour, Kenya, where the main power generator is well run, with prices regulated by government but the company is listed on the KSE which allows it freedom raise funds and pursue market opportunities without too much interference (see www.kengen.co.ke/index.asp). By way of example, while Kenya is suffering from the same drought as TZ and Uganda, they were able to export power to Uganda to help them in their drought related electricity shortfalls!
1
Electricity supply is old technology, inasikitisha kwamba in this day and age - the information age -that we live in sisi waTanzania,who have the right climate for progress which other countries are not blessed with, bado tunababaika na mambo ambayo on the face of it can be dealt with quite easily as they are not insurmountable.
1
Lets remember this when we next exercise our democratic rights at the polls.
1
I hope you have a "brighter" 2007 - happy new year!
1
Salaam
1
Majaliwa