Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi
- Posti ya ukaribisho katika blogu ya Mh. Zitto Kabwe
Zaidi bofya hapa.
Natafuta tafuta wabunge wengine wanaoblogu – bila bila mpaka sasa...
Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi
- Posti ya ukaribisho katika blogu ya Mh. Zitto Kabwe
Zaidi bofya hapa.
Natafuta tafuta wabunge wengine wanaoblogu – bila bila mpaka sasa...
Mkutano wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010 uliofanyika mjini Santiago, Chile ulipita vizuri. Nilibahatika kukutana na wanablogu wawili wa Tanzania, Christian Bwaya na Deogratias Simba ana kwa ana kwa mara ya kwanza.
Ilikuwa ni furaha tupu kwani tuliweza kuzungumza mengi kwa lugha yetu na kwa kuelewana vizuri bila ufafanuzi au maelezo mengi kama vile tunapoongea na watu kutoka nchi na tamaduni tofauti.
Katika siku zile mbili za mkutano watu wengi kutoka kila bara walieleza na kutushirikisha katika miradi yao ya uanablogu au uanahabari wa kiraia. Wengi wa watoa mada walitoka katika nchi zenye ahueni katika upatikanaji wa intaneti, yaani hawategemei migahawa ya intaneti au kompyuta za wanapofanyia kazi ili kublogu na kuendesha miradi hiyo na hivyo miradi yao ilionekana kuwa na mafanikio zaidi. Hata hivyo kutoka Afrika kuna nchi kama Liberia na Madagaska ambazo zimeweza kufanikisha miradi hiyo ya uanahabaro ewa kiraia katika hali ngumu kama yetu au pengine hali mbaya zaidi. Maelezo ya miradi hiyo pamoja maelezo mengine ya mkutano yamewekwa hapa.
Pamoja na mambo mengine mimi binafsi nilijifunza mengi katika mkutano ule. Pengine neno ‘nilijifunza’ halitoi maana sahihi, ninaweza kusema kuwa nilithibitisha hisia zangu za muda mrefu. Kwamba ili jambo lolote au juhudi yoyote iweze kufanikiwa panatakiwa kwanza pawe na visheni, nia, ikesha mipango inayoeleweka kadhalika panatakiwa pawe na ufuatiliaji mzuri na usiokoma-koma. Mambo ya bahati bahati yanawezekana kutokea lakini sio mara nyingi bahati inaweza kuzaa mafanikio ya kudumu ambayo yanaweza kubadilisha jamii au kumpa mtu au jamii nafasi inayoheshimika.
Simba, Bwaya na washikaji wa Kibangladeshi wakiwa Sao Paulo, Brazil
Simba akisikiliza au kushangaa jambo wakati wa mkutano
Picha nyingine za mkutano
Jengo la maonyesho (Theatre/Opera house) mtaa wa Augustina.