Wednesday, January 06, 2010

'I saw it too' commented Sister Maria 'it was not human and must have been a spirit. The students later told me it was Michael Jackson'.

Michael Jackson’s ghost sighted in Zimbabwe

Africa News

Wednesday, October 21, 2009

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI – Tanzania

Tanzania imepanda kwa chati kwenye takwimu mpya zilizotelewa muda mchache uliopita.. Ipo kwenye alama ya 62 kati ya nchi 175 zilizoangalia kwenye chati ya Reporters Without Borders For Press Freedom.

Chati hiyo inaangalia uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari katika nchi 175, na kiwango ambacho mamlaka za nchi zinathamini, zinahakikisha au kiwango ambacho zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari, pamoja na jitihada zinazofanywa na mamlaka katika nchi ili kuhakikisha kuwa uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari unaheshimiwa.

Monday, September 14, 2009

Binaadamu na Mashine

Kama ilivyoandikwa kwenye hii blogu, kutafsiri kiswahili kwa kutumia mashine au komyuta pekee ni kazi ngumu.


Kuna mtu katuma maoni kwenye blogu – kwa Kiswahili na Kiingereza. Nadhani alitafsiri kwa mashine:

Comment:


Kiswahili
Kama hii barua pepe yangu fika, ninyi tafadhali vidarebefordra barua pepe ya risiti yangu.
Mimi vidarebefordra email hii kwa nchi mbalimbali duniani moja 1,000 kwa siku.
Kama wewe ya maambukizi ya ujumbe wa barua hii tafadhali samarbeta.

Ujapani redio zuliwa silaha
sana katika ulimwengu wa kwanza miaka 60 iliyopita. Japan na USA ikawatoa kampuni ya kigeni kwa sababu ya redio ya silaha. Japan na USA alifanya siri vita (uhalifu) katika redio moja sidedly silaha katika nchi mbalimbali duniani. Na Japan na Marekani kuwa nchi ya viwanda nafasi ya kwanza duniani. Japan na Marekani kuwaangamiza economy.There kigeni ni redio ya silaha katika nchi yoyote ya mahali sasa. The Kijapani redio silaha ni halina nguvu. Nchi yako lazima kulipiza kizazi kwa Japan na Marekani, kampuni ambayo ni kubwa kuliko Kijapani na american nusu ni kitu ya nchi yako. Wote wa Kijapani na makampuni ya Marekani ni mambo ya nchi mbalimbali duniani. Dunia lazima kulipiza kizazi kwa Japan na USA mpaka kampuni ya kutoweka kutoka Japan na USA Mei wewe kusamehe siri vita kwa muda mrefu kuwa Japan na Marekani walitumia silaha kwa redio? Ni hauhitaji silaha na kuanguka katika Ujapani na Marekani Don't kununua bidhaa na gari (Toyota • Nissan • Honda • Suzuki • Mitsubishi • Ford • GM • USAcar) • Umeme (National • Matsushita • HITACHI • Sanyo • NEC • Sony • PIONIEER • Sharp • Victor • wengine) zinazozalishwa nchini Japan na USA! Ikiwa kuwafundisha mataifa yako yote katika barua pepe na simu na wengine, Japan na USA kuanguka kwa njia zote.
Na makampuni ya nchi yako kuongezeka.

Kama USA majani Ujapani, Asia kuharibiwa na viwanda ni vita, na ulimwengu sekta ya mafanikio.

Ni lobsters yoyote, na nyangumi hukua. Ujapani tu hawakupata Valar na exterminated ya Valar kutoka duniani. Kama kwa miaka mia kadhaa, wewe kushika whaling kukataza ya uvuvi na lazima dunia kufanya bahari nyangumi rikedom. Nyangumi wanaweza kula moja kwa moja.

Anyway, lazima kulipiza kizazi dhidi ya Japan na USA ni mpaka katika kampuni ya nchi yako katika Ujapani na kampuni ya Kimarekani ambayo You got kwa siri vita mpaka kuja it-matajiri na nyangumi wa ulimwengu tena bahari.

Please translate this email ndani yako lugha ya kitaifa, na kuruhusu Unaweza kuonyesha mataifa yote ya nchi yako, na kushirikiana.
Kama inawezekana katika nchi ya kigeni ya barua pepe tafadhali samarbeta.

Katika Kijapani Serikali, email nchi ya kigeni ni blocked kuficha ubaya wa Kijapani tendo. Mimi kuanzisha free mail (yahoo / goo / Excite / infoseek / moto), na email nchi ya kigeni ni kuzuiwa kwa mara kadhaa. Tafadhali tuma barua pepe hii hapa chini ya anwani kutoka nchi yako.

English
If my this email reaches you, you please transmit an email of the receipt to me.
I transmit this email to the various countries in the world 1,000 on one day. As for you of the transmission of a message of this email please cooperate.

Japan invented the radio weapon very first in the world 60 years ago. Japan and U.S.A. gave up a foreign firm because of a radio weapon. Japan and U.S.A. did secret war (a crime) in a radio weapon one-sidedly in the various countries in the world. And Japan and U.S.A. became the industrial country of the first place world. Japan and U.S.A. destroyed foreign economy.There is the radio weapon in country of any place now. The Japanese radio weapon is powerless. Your country must retaliate for Japan and U.S.A. The company where is higher than Japanese and american half is a thing of your country. All the Japanese and American companies are things of various countries in the world. The world must retaliate for Japan and U.S.A. till a company disappears from Japan and U.S.A. May you forgive the long secret war that Japan and U.S.A. used a radio weapon for?  It does not need the weapon to collapse in Japan and U.S.A. Do not buy a product and a car (ToyotaNissanHondaSuzuki
MitsubishiFordGMU.S.A.car)ElectricityNational Matsushita Hitachi SANYO NEC Sony PIONIEER SHARP Victor othersproduced in Japan and U.S.A.!  If you teach all your nations it in email and telephone and others, Japan and U.S.A. fall by all means.
And the companies of your country increase.
If
U.S.A. leaves Japan, the Asian industry is destroyed by war, and the world industry prospers.
It is in lobsters anything, and the whale grows. Only
Japan caught whales and exterminated the whales from the world. As for several hundred years, you keep the whaling prohibition of fishing and must make the world sea whale richness. The whale can eat directly.
Anyway, you must retaliate against Japan and U.S.A. till it is it in the company of your country in Japan and the American company which You got by secret war till come to it-rich with a whale the again world sea.

Please translate this email into your national language, and let You show all nations of your country it and cooperate. If possible in the foreign country of the email please cooperate.
In the Japanese Government, the email to the foreign country is blocked to hide a Japanese evil deed. I establish free mail (yahoo / goo / excite / infoseek / hot), and the email to the foreign country is prevented with several times. Please send this email to an address below from your country.




Friday, May 09, 2008

WAGONJWA JEURI

Tuko tayari kutumia jeshi letu la majini kukusanya waliopoteza maisha, waliopotea, na kuweka hali sawa. Lakini ili kuweza kufanya hivyo, utawala wa kijeshi lazima uturuhusu kuingia nchini humo.
2008

Tunaghafirishwa na serikali ya Myanmar kwa inavyojivutavuta kupokea na kukubali usaidizi wetu. Ni wazi uwezo wa serikali hiyo siyo mkubwa kuweza kukabili hali iliyopo, ambayo ni janga"
2005

"Madaktari wetu wanao uzoefu wa kimataifa na wanaijua lugha ya kiingereza ambayo itawawezesha kuwasiliana na waathirika. Tupo tayari, tunasubiri tu majibu ya serikali ya Marekani."

Friday, May 02, 2008

MANDELA BADO NI GAIDI MAREKANI

"Afrika ya kusini ni nchi ambayo tuna mahusiano mazuri nayo kwa sasa, ni jambo lanalotia aibu kwamba inanibidi kuondoa kikwazo cha pingamizi la kibali cha kuingia nchini (cha viza) kwa mwenzangu, waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya kusini, na hata kwa kiongozi mashuhuri Nelson mandela,"

- Condoleeza Rice, akitetea muswada wa kuwaondoa viongozi wa chama tawala cha Afrika ya kusini, ANC, katika orodha ya vikundi vya kigaidi.

Mpaka sasa wanachama wa ANC huwa wanahojiwa kwa undani wanapotaka kuingia Marekani. Mwaka 2002, mwenyekiti wa ANC Tokyo Sexwale alinyimwa visa. Mwaka jana aliyekuwa balozi wa Afrika ya Kusini umoja wa Mataifa tangu 2002 mpaka 2006, pia alikataliwa visa ya kwenda kumuuguza nduguye mpaka baada ya huyo ndugu alipofariki dunia.

Sunday, April 20, 2008

MAHOJIANO NA THOMAS MAPFUMO


Thomas Mapfumo, mwanamuziki aliyehamasisha vita ya ukombozi wa Zimbabwe anadai kwamba Komredi Mugabe angeshakubali kuachia ngazi na kuwapa MDC uongozi wa serikali Zimbabwe. Anasema tatizo ni kwamba maswahiba wa Mugabe hawatamruhuzu mzee akubali kushindwa kwa vile wanahofia kushitakiwa kwa kukiuka haki za raia na serikali mpya ya MDC. ..

Mapfumo yuko ziarani Australia. Niliongea wiki iliyopita kuhusu muziki wake pamoja na siasa ya Zimbabwe.

Bofya hapo chini usikilize mahojiano hayo yaliyowezekana kwa hisani ya kipindi cha Afroworld ndani ya Radio Adelaide.











MYKAL ROSE


Mahojiano na Mykal Rose ndani ya mrindimo wa dub - kwa hisani ya Abdalla Ezza.
Zawadi yako Rasta.















Tuesday, November 06, 2007

RISING VOICES

Kama unapenda kusaidia wengine wajue jinsi ya kublogu ili kuhabarisha umma au kuweka video kwenye mtandao Rising voices wanaendelea kutoa kutoa senti zitakazokurahisishia kufundisha wengine.

Unaweza ukapata dola 5000 zitakazokuwezesha kufundisha wengine. Unachotakiwa kufanya ni kutuma maombi kwa jamaa wa raising voices. Mstari mfu ni novemba 30, 2007.

Fanya utume. Bofya hapa kwa maelezo zaidi. Fomu za maombi zipo mwishoni mwishoni mwa ukurasa.

Mtazamo mbadala: Shivji ahoji tuzo ya Mo Ibrahim

Kwenye kurasa za Pambazuka kuna mawazo mbadala ya Profesa Shivji kuhusu tuzo ya utawala bora aliyopewa Chissano. Na kabla ya Shivji kupandisha makala yake, mwanazuoni Horace Campbell alikwishapandisha nyingine siku chache kabla.

pamoja na mengi mengine Shivji anaanza:

"Mo Ibrahim’s prize for a retired African president which was awarded to Joachim Chissano of Mozambique was in my view an insult to the African people." Issa Shivji raises a number of questions around the award such as how and what is "good governance" and why is it only applied to Africa? And most importantly "for which and whose democracy they are getting a prize".



Horace Campbell kaandika kirefu zaidi:

According to the media, "Mo Ibrahim, a Sudanese-born telecommunications entrepreneur, established the prize as a way of encouraging good governance in a continent blighted by corruption and a frequently loose adherence to democratic principles." Not a word is mentioned about the living conditions of the people of the Sudan from where Mr. Ibrahim hails…..

But, isn’t this prize also a sign of the political retrogression in Africa? The idea of a President voluntarily stepping down is now so novel in the face of leaders such as Museveni and Mugabe that Chissano indeed stands out. Compared to Robert Mugabe and Thabo Mbeki, and their megalomanic policies, Chissano does look good.

While announcing Chissano as the winner, Kofi Annan may have gone overboard by saying, "leadership should be the ability to formulate a vision and to convince others of that vision. It should be the skill of giving courage to accept difficult changes to make possible a longer term aspiration for a better and fairer future."

Sunday, September 23, 2007

TOA MAONI - PENDEKEZA BLOGU BORA AFRIKA


Wanablogu - Msisahau kutembelea katika blogu ya JUMUWATA ilikuchangia, kukosoa, kuongezea na kuupa muelelekeo mkamilifu muelekeo wa JUMUWATA.


Dondoo za katiba ziko ndani ya blogu ya JUMUWATA, hivyo maoni ya wengi yanahitajika ili isije ikawa ni watu wachache wameamua tunaenda wapi.


Mchango wa wanablogu wenye blogu na wasio na blogu unahitajika ilikuwa na kitu kikamilifu kabla ya kwenda kwenye hatua nyingine.




Mapendekezo ya blogu bora Afrika yanafikia mstari mfu tarehe 30 mwezi wa Tisa.


Katika mapendekezo kutoka kila pande za dunia Afrika haina blogu zilizopendekezwa - wakati nikiandika. Kuna ukame kwenye nchi za Afrika - hakuna hata alama moja ya blogu iliyopendekezwa.


Kama kuna blogu inayoandikwa na Mwafrika ambayo inakukuna moyo fanya uipendekeze ndani ya ukurasa huu.


Hapa chini ni maelezo ya kimombo:


Best of the Blogs: Deutsche Welle
Nominate your favorite blogs today! You're a blogger? You know a good blog? You like blogs, videoblogs and podcasts and want to share your favorites with the world?


Well, you've come to the right place. The BOBs -- short for the Best of the Blogs -- are here to keep track of the world's most interesting Weblogs, podcasts and videoblogs, and we need your help in doing it.


Suggest your favorites


You have until September 30 to head over to the suggestion form and give us the lowdown on all the blogs that glue your eyes to the screen and the podcasts that make you keep your headphones on. You can choose from the following categories:


Best Weblog, Best Videoblog, Best Podcast, the Blogwurst Award, Best Weblog /(Insert contest language here) and the Reporters Without Borders Award. In addition to the overall world's Best Weblog, another award will be given to the Best Weblog in each of the BOBs' 10 official languages making for 15 different prizes.


Who gets to play along?


The Deutsche Welle's Best of the Blogs awards are open to any blog, podcast or videoblog in Arabic, Chinese, Dutch, English, French, German, Persian, Portuguese, Russian or Spanish and meet the criteria. Read through the Road Map to find out more of the competition's details.


The people making the decisions


First and foremost, the BOBs are about the Weblogs (and 'casts) you submit, a blog you that is never entered into the contest can never win -- so get to work. When the submission window closes on Sept. 30, the BOBs jury of bloggers, podcasters, journalists and media experts will begin their work.


If your not impressed with the jury members' biographies, then keep an eye on the BOBs Blog, where they will have a chance to stun you with their insight and analysis. And please also check out the sponsors and media partners who are helping make the third annual Best of the Blogs possible.

Thursday, September 13, 2007

Madhumuni ya tangazo la biashara kwanza ni kuvutia na kushika jicho la mnunuzi. Kwa hilo jamaa wa American Apparel wameweza - kushika jicho.

Cha kushangaza, hivi hawakuweza kupata mrembo mkubwa kwa umri kidogo, halafu akasitiri kidogo kifua chake, ambaye wasingempaka masizi kumfanya awe mweusi tii. Nijuavyo Marekani kuna weusi tii kwa wingi.

Sina hakika mlengwa wa biashara hii ni nani, japo tangazo limezua gumzo.

Tuesday, August 28, 2007

MWANZO WA MWISHO WA SIASA ZA RAFU?

"Zitto amekuwa Zitto, wapinzani sasa wamepata hoja, wametuzidi katika hoja, tunapaswa kuchagua viongozi walio bora ili (wapinzani) wasituzidi katika hoja.

"Inashangaza Zitto ambaye amepewa ‘red card’ bungeni kushabikiwa na idadi kubwa ya Watanzania wakiwemo wana CCM ambao walikwenda Jangwani kumlaki na kumsikiliza wakati akitokea Dodoma, ni lazima tukisafishe chama ili wapinzani wasije kutupiku,"

- Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Kapteni Jaka Mwambi
DAIMA, 27-08-2007
Hoja bin hoja kama hivi tutafika kwenye hoja bin haki, akina Zitto wasikome kuzua hoja tutoke kwenye siasa za pilau anazosema JK hapa.

Sunday, August 19, 2007

Australia imefukuza watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe

Hatimaye serikali ya Australia imeitikia wito uliotolewa mwezi wa nne mwaka huu na gazeti la Zimdaily, wa kuwafukuza watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe ambao wanasoma ughaibuni kama njia mojawapo ya kuwaadhibu viongozi hao.

Adhabu hiyo imetolewa wakati viongozi wa SADC huko Zamnbia wakiwa wakikubaliana kwamba hali ya Zimbabwe sio mbaya kama wamagharibi wanavyodai. Maamuzi ya Australia na yale ya viongozi wa SADC yanafuatana kama vile mabodia wanavyotupiana masumbwi moja baada ya jengine.

Wakati zoezi la kuwataja kwa majina, pamoja na anwani za wanapoishi watoto wa viongozi wa serikali ya Zimbabwe lilipozuka mwezi wa nne mwaka huu - zoezi liliondaliwa na gazeti la Zimdaily msimamo wangu ulikuwa: sioni haki ya binaadamu mmoja kushinikizwa kwa kutumia binadamu mwingine. Kwamba ikiwa baba yangu ana makosa fulani basi na mimi nihukumiwe kwa makosa yale.

Nilitundika maoni pale kwa Jikomboe, wengine walikuwa na mawazo tofauti. Nikichukulia mfano, kama mimi ningekuwa mmojawapo wa watoto wale, mwenye mawazo tofauti na baba yangu, pengine nimetumia skolashipu iliyoangalia uwezo wangu wa kimasomo, na ninafanya vizuri tu shuleni, halafu nizuiwe kuendelea na masomo kwa sababu baba yangu anafanya kazi serikalini… Haki yangu ya kuishi kama mtu huru itakuwa iko wapi.

Ninaelewa haki ya taifa lolote kuwa na uamuzi ni nani anayeweza kuishi katika mipaka yake nabaki na tatizo la kuelewa dhana ya haki za kibinadamu katika hili.

Friday, July 20, 2007

FIMBO YA MBALI INAUA NYOKA

Fimbo ya mbali inaua nyoka. Hizi zama za teknolojia za mitandao ya intaneti zinabadili mambo.
1
Jioni hii baada ya kazi nafungua barua pepe nakutana na tangazo la mkanda mfupi wa muziki wa Ras Nas. Na hivi ndiyo kwanza nimemaliza kuangalia na kusikiliza muziki wa Ras Nas - muwakilishi wa sanaa toka Tanzania.
1
Muziki timilifu kila upande. Anaanza kwa muziki mwororo wa miondoko laini ya rumba ila sebene lililofuata limeniamsha kitini. Ningekuwa na utaalamu wa youtube kama Kitururu ningepandisha filamu. Lakini si haba, kuna kiungo hapa ukibofya utafika kwenye hiyo filamu ya Ras Nas.
1

Halafu nasoma barua pepe nyingine nakutana na kiungo kingine cha muziki wa Tanzania: Chemundu & Mbega Arts. Japo hakuna filamu ya kikundi wala sauti kwenye tovuti - napata ujumbe kuwa sanaa Tanzania inatokota kisawasawa. Kwa maelezo yao:
1
Chemundu na Mbega Arts ni kikundi cha muziki wenye vionjo vya muziki jadi(asili) halisi wa Tanzania na pia kuchanganya na mitindo ya Kimataifa kama:pop,afro rhumba na afro jazz.
Mbega Arts ilianziswa na mwanamuziki maarufu Che Mundugwao " chem ". na kujumuisha wanamuziki na wasanii wa muziki wa jadi vijana wenye vipaji vya hali ya juu ,ambao wameshawahi kushiriki katika ziara na matamasha mbalimbali ya kitaifa(tamasha la sanaa Bagamoyo) na kimataifa katika nchi za Kenya,Sweden,Denmark,Finland,Uingereza.n.k
1
Hiyo isitoshe, ndani ya barua pepe nyingine nakuta jamaa wa Afropop Worldwide wanaitangaza Tanzania kinamna. Moja ya santuri wanazocheza katika juma la muziki wa Afrika (African Summer Dance Party) inatoka kwa bendi ya Tanzania FM Academia. FM wamewekwa bega kwa bega na Hugh Masekela na Ricardo Lemvo katika chaguo la wataalamu wa AfroPop.
1
Nimeshapata mshawasha, ngoja nielekee kwenye miziki mjini - kuna rege mitaa ya kati huko. Ijumaa hii silali ndani. Fimbo ya mbali ishanichapa.

Tuesday, June 26, 2007

Nyerere Press Conference - 14 March 1995

"Any government that works for the wealthy does not collect tax, it chooses to harass small-time dealers,"

"Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption,"

"This would not only lead to collapse of the now-sensitive 30-year-old union between the twin-islands of Zanzibar and Pemba and Tanzania mainland, but would also plunge the country into chaos," (talking about condoning religious differences and tribalism)

Monday, June 11, 2007

SEMBENE OUSMANE AFARIKI DUNIA


Muasisi wa utengenezaji filamu barani Afrika, Sembene Ousmane amefariki dunia mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 84.


Sembene ndiye mwafrika wa kwanza kutengeneza filamu barani Afrika. Alikuwa mmojawapo wa wa waanzilishi wa tamasha la filamu Afrika, FESPACO. Alikuwa pia ni mtunzi wa vitabu. Kwa wale waliosoma somo la kiingereza wakiwa sekondari bila ya shaka walisoma pia kitabu cha God's Bits of Wood alichokiandika huyu mzee.


Binafsi nilivutiwa na kitabu hicho. Kadhalika nilivutiwa mno na filamu yake ya mwisho aliyoitengeneza, Moolaade. Mara baada ya kuiangalia nilieleza utamu wake kwenye blogu hii takriban miaka miwili hivi iliyopita.


Ameacha pengo lisilozibika - au pengine akiwa kama alama ya zama za filamu za mwanzo barani Afrika pia anafunga pazia la zama hizo - hasa kutokana na mabadiliko ya haraka yanayotokea katika utengenezaji na hadhira ya filamu za kiafrika barani hivi sasa.

Friday, June 01, 2007

MRADI WA KUIMARISHA SHUGHULI ZA BLOGU

(Maggid Akiwa katika outreach projects. picha na Maggid Mjengwa)
1
Global Voices hivi sasa wanapokea proposals za miradi ya uimarishaji shughuli za blogu. Bila ya shaka wengine wetu wameshaanza shughuli hii ya uimarishaji uandishi wa kiraia bila ya msaada wowote.

Hata hivyo haidhuru kama utapatikana msaada zaidi kidogo ili kurahisisha mambo.

Endelea hapo chini, kama unaweza kufuatilia kabla ya tarehe 15 juni fanya harahara.

Application Deadline: June 15, 2007

Rising Voices, the outreach arm of Global Voices, is now accepting project proposals for the first round of microgrant funding of up to $5,000 for new media outreach projects. Ideal applicants will present innovative and detailed proposals to teach citizen media techniques to communities that are poorly positioned to discover and take advantage of tools like blogging, video-blogging, and podcasting on their own.
As the internet becomes more accessible to more people, as computers become cheaper, and as software applications move from the desktop to the web, the so-called digital divide seems to be narrowing. In its place, however, we see a participation gap in which the vast majority of blogs, podcasts, and online video are being produced in middle-class neighborhoods in major cities around the world.
Rising Voices aims to help bring new voices from new communities and speaking new languages to the conversational web, by providing resources and funding to local groups reaching out to underrepresented communities. Examples of potential projects include:

  • Purchasing an affordable digital video camera and teaching a group of rural students how to produce an ongoing video-blog documentary about the lives of their grandparents.

  • Organizing a regular workshop on blogging and photography at a local orphanage. Portions of the budget could be used on cheap digital cameras and internet cafe costs so that participants could describe their local neighborhoods to a global audience with text and photos.

  • Working with a local NGO or social entrepreneur so that their challenges, successes, and stories are told to a global audience.

  • Translating our new media curriculum to an indigenous language, like Quechua or Wolof, that is currently not represented in the blogosphere or "podosphere." Then use the learning modules to encourage bloggers to write in those languages.


The sky is the limit, but unfortunately funding is not. Rising Voices outreach grants will range from $1,000 to $5,000. Please be as thoughtful, specific, and realistic as possible when drafting your budgets.


Feel free to ask questions in the comments section below or by sending an email to
outreach@globalvoicesonline.org

Kiungo chenye habari nzima kipo hapa.

Monday, May 07, 2007

CHEMA HAKIDUMU

Chema hakidumu kingekupendeza
Ungawa na hamu kukingojeleza
Saa ikitimu kitakuteleza


Chema wangu babu Kibwana Bashee
Alojipa tabu kwamba anilee
Illahi Wahabu mara amtwee


Hizo beti mbili nilizikariri zamani kutoka kwenye kitabu cha Abdilatif Abdala "Sauti ya Dhiki". Na kama ninavyozikumbuka zimekuwa zinanizinga mawazoni kwa masiku kadhaa sasa.

Nimeingiwa na machungu na woga. Uwezo wangu wa kufikiri au kutatua matatizo yaliyonifika umeniponyoka. Maisha yamenikumbusha uwanaadamu wangu. Kinachonisukuma ni ule moyo wa stahamali tu. Na ninaomba nijaaliwe stahamali zaidi.

Kitambo kidogo kilichopita Mwenyezi Mungu alimtwaa kipenzi Mama yangu Mkubwa, Kadala. Marehemu Kadala nilikuwa naye karibu sana wakati wa utoto wangu.

Naam, ndio maisha. Na hapa nilipo maisha mengine yanaenda kwa kasi ya mwendo wa radi. Nakimbiakimbia, ninachakurachakura kama kuku kutwa nzima. Kukicha naanza tena kama jana. Ndio maisha.

Basi naona bora kukawia kuliko kuiwacha safari. Tupo wote safarini japo tunaonana kwa nadra bloguni. Mambo yakisawazika bila ya shaka nitaongeza kasi na huku kwenye mitandao pia.

Haidhuru. Kule kwenye kurasa za Global Voices baada ya muda kama mwezi hivi kuna muhtasari wa blogu za kiswahili uliopandishwa leo. Tafadhali tupa jicho na huko pia. Bila kusahau kuperuzi kidogo kwenye ukurasa wa Reuters Tanzania.

Saturday, March 10, 2007

WOMADELAIDE 2007

(wazawa wa Adelaide - Kaurna - wakibariki tamasha)
1

Wikiendi hii tumerejea tena kwenye moja ya matamasha maarufu ya muziki wa kimadunia katika Australia - Womadelaide 2007. Mwaka huu tamasha hili ni la 15 hapa Adelaide na kwa mara ya kwanza kumekuwa na ratiba tofauti. Katika siku tatu za tamasha hili wanamuziki wote vinara wanatumbuiza mara moja tu. Haidhuru.
1
Bila kujali joto la kiangazi wapenzi wasiopungua 70 elfu wameshaanza kuburudika ndani ya viwanja vya Adelaide botanic park na wataburudika kwa siku tatu mfululizo mpaka nyasi kugeuka vumbi.
1
Pamoja na wanamuziki wa Kiafarika kama Femi Kuti (Nigeria), Salif Keita (Mali) na Mahotella Queens (Afrika ya Kusini) magwiji wengine kutoka pande zote za dunia kama akina Asha Bhosle (India); Kronos Quartet (US); Blue King Brown (Australia); Gotan Project (France / Argentina); Lior (Australia); Lunasa (Ireland); Emma Donovan Band (Australia); na Mariza (Portugal) watatumbuiza pia.
1
Kwa upande wangu mpaka hivi sasa nimeshahudhuria maonyesho ya bendi mbili za kutoka Afrika: Mahotella Queens na Femi Kuti and the Positive Force. Na bila ubishi wowote Mahotella Queens wamenisuuza moyo vilivyo.

(Bi mkubwa wa ki-Kaurna akisoma risala ya kubariki tamasha na kuwaenzi wenye nchi)
1
Kama ilivyo mila na desturi ya hapa Australia haianzi shughuli bila kutoa heshima kwa wazawa wa nchi hii wanaotambulika kama Ma-aborijino au Indigenous people ambao walikuwa 'hawatambuliki' kama binaadamu kamili kabla ya mwaka 1967.
1
Wazawa walianza kwa kutoa heshima ya ki-kaurna (inatamkwa ga-na). Mzee wa kabila (kama anavyoonekana pichani) alianza kusoma dua za kikwao akafuatiwa na vijana waliocheza ngoma ya kubariki tamasha. (juu kabisa pichani)

MAHOTELLA QUEENS (Womadelaide 2007)

(Mahotella Queens - Womadelaide 2007)
1
Mahotella Queens ndio waliofungua dimba ya tumbuizo kwenye tamasha la 15 la Womadelaide. Baada tu ya baraka za ufunguzi, bila kuchelewa kikosi cha maajuza watatu kutoka Afrika ya kusini, Mahotella Queens walivamia jukwaa namba moja na kuporomosha vibao vyao vyote maarufu - pamoja na Kazet na Umuntu Ngumuntu. ilikuwa onyesho kabambe - kwa lugha ya wanamiziki wanasema walipiga "tight set".
12
Miye naona hii ni baraka kuwashuhudia maajuza hawa wakitumbuiza, kwani walisharitaya shughuli za muziki baada ya kupotelewa na wanamuziki wenzao watatu wakiwemo Mzee Mahlatini na West Nkosi. Naona ni baraka vile hawa madada wazee - Hilda Tloubatla, Nobesuthu Shawe Mbadu na Mildred Mangxola ndio historia ya muziki wa dansi wa Afrika ya kusini. Hawa ndio hasa waliokuwamo kwenye kuipika mbaqanga jive.
1
Na kama alivyokuwa akieleza Bibie Hilda Tloubatla akiwa jukwaani - bila kujituma, kukaza nia tena baada ya kukata tamaa na misiba pengine wasingelikuwapo ndani ya tamasha mwaka huu.

Shoo yao ilikuwa swafi sana - walikuwa na mpigaji gitaa zito, mpiga gitaa, mpiga ngoma (yaani "drums") na mpiga kinanda tu. Hata hivyo vibibi hivi vilitoa vichekesho na mawaidha kwa wanawake na wanaume.
1
Usia ambao pengine haukuwafikia vizuri watoto wadogo na vichwa maji wengine ni pale walipowaambia akina mama: "Mkitaka kuwa na afya na furaha, muweze kucheza kama sisi mpaka uzeeni, siri ni kujidamka alfajiri ya saa kumi, umpe mumeo staftahi, na akirejea kutoka kazini akute maakuli, basi mumeo mwenyewe atakuwa akiwahi kurudi nyumbani kila siku, na kama ana uwezo atakununulia chochote unachotaka". Ma-feminist walinung'unika na kauli.